Tangaza hapa

e

Featured Posts

Tuesday, 26 May 2015

Maradona adai Rais wa shirikisho la mpira wa miguu duniani, FIFA ni dikteta wa kutupwa.

Unknown     05:59    



 Rais wa FIFA wa sasa Sepp Blatter hana mpinzani baada ya wagombea wenzake wanaowania nafasi hiyo kujiondoa kwa madai uchaguzi huo umegubikwa na rushwa zaidi badala ya haki.

Uchaguzi huo umepangwa kufanyika  kufanyika leo May 26 huko jijini Zurich, Uswis.

Baadhi ya wadau wa soka duniani wamekua na mitazamo hasi kuhusiana na Rais huyo kuendelea kuongoza Shirikisho hilo kwa mara nyingine huku mkongwe wa soka kwa mara nyingine Maradona akimvaa Sepp Blatter kwa kumuita kuwa ni kiongozi wa mabavu.

Kauli ya Maradona imekuja baada ya FIFA kutengeneza mazingira mazuri ya Rais huyo kuongoza tena na kudaiwa kuwepo mazingira ya rushwa ambayo mwenyewe ameyaita ni ya udhalilishaji.

Alisema kwa miaka ya sasa mchezo wa mpira wa miguu umebadilika na kujaa siasa pamoja na rushwa na FIFA wamekua wakiukandamiza kwa kuendekeza rushwa kwa kiasi kikubwa.

0 comments :

Top headlines

© 2011-2014 MICHEZONI. Designed by Alfred Meshack Bloggertheme9. Powered by Blogger.