Tangaza hapa

e

Featured Posts

Sunday, 24 May 2015

Martin Odegaard aweka rekodi ya kuwa kijana mdogo kabisa kucheza la liga.

Unknown     17:18    

Odegaard ambae hadi sasa ana umri wa miaka 16,miezi 5 na siku 6 alijiunga na Madrid akitokea timu ya Stromsgodset mwezi wa kwanza mwaka huu.

Kinda huyo kutoka Norway  amewekaka rekodi hiyo ya kuwa kijana mdogo kabisa kucheza la liga,akiwa na umri wa miaka 16 tu .

Kiungo huyo aliingia kutokea benchi na kuchukua nafasi ya mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo dakika ya 58 katika mchezo wa kufungia msimu uliopigwa pale Santiago Bernabeu dhidi ya Getafe jumamosi .

Alimbadili Cristiano Ronaldo baada ya kuwa na msimu mbovu kabisa ambapo wameshindwa kuchukua kombe lolote msimu huu hadi unaisha.

Odegaard alicheza mechi yake ya kwanza akiwa na umri wa miaka 15 na kuwa kijana mdogo zaidi wa Norway kucheza mechi za kimataifa pale alipoanza dhidi ya United Arab Emirates akiwa na umri wa miaka 15 na siku 253 mwezi wa nane mwaka jana, na alivunja rekodi iliyokaa zaidi ya karne moja

0 comments :

Top headlines

© 2011-2014 MICHEZONI. Designed by Alfred Meshack Bloggertheme9. Powered by Blogger.