Katika msimu wake wa kwanza
Bernabeu, Ancelotti alishinda ligi ya mabingwa, Copa del Rey, Uefa
Super Cup na kombe la klabu bingwa ya FIFA duniani.
Real Madrid imevunja mkataba na kocha wake huyo baada ya kuinoa kwa miaka miwili.
Ancelotti ameshindwa kushinda medali msimu huu na kumaliza pointi mbili nyuma ya mabingwa FC Barcelona.
Kocha wa Napoli Mhispaniola, Rafael Benitez anapewa nafasi kubwa ya kuchukua mikoba ya Ancelotti.
Rais wa Real Madrid, Florentino Perez amethibitisha kufukuzwa kwa Carlo na anatarajia kutangaza mrithi wake juma lijalo.
Kocha huyo Muitaliano anatazamiwa kuchukua mikoba ya Manuel Pellegrini kama klabu hiyo itaachana naye baada ya kocha huyo pia kuwa na msimu mbaya hapo Etihad.
Kocha huyo Muitaliano anatazamiwa kuchukua mikoba ya Manuel Pellegrini kama klabu hiyo itaachana naye baada ya kocha huyo pia kuwa na msimu mbaya hapo Etihad.
0 comments :