Taarifa iliyoporipotiwa na Saleh Ally inasema kwamba kiungo mpya wa Yanga, Deus Kaseke ameongezwa katika kikosi cha timu ya taifa kinachojiandaa kuivaa Misri.
Kaseke ambaye amesajiliwa na Yanga siku chache zilizopita kwa dau la Sh milioni 35 akitokea Mbeya City FC,yuko pamoja na wachezaji wengine watatu walioongezwa katika kikosi hicho.
Wachezaji hao wote wameanza mazoezi leo kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.
Wengine walioongezwa katika kikosi hicho ni kipa wa Mtibwa Sugar, Said Mohammed 'Nduda" pia beki wa timu hiyo Andrew Vincent na kiungo wa Azam FC, Gardiel Michael.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij ambaye amekalia kuti kavu kutokana na kikosi chake kwenda mwendo wa kusua, ameamua kuimarisha kikosi chake na imeelezwa atafanya mchujo kabla ya kwenda Misri.
0 comments :