Tambwe alijiunga na Yanga Desemba mwaka jana baada ya kutemwa na
Simba na ameifungia timu hiyo ya Jangwani mabao 13 kwenye mechi za ligi
na mengine matatu katika mechi za kimataifa.
Jumla Tambwe ana mabao 14 (moja alifunga akiwa Simba) kwenye mechi za ligi na ni wa pili kwa ufungaji, anaongoza Simon Msuva mwenye mabao 17.
Jumla Tambwe ana mabao 14 (moja alifunga akiwa Simba) kwenye mechi za ligi na ni wa pili kwa ufungaji, anaongoza Simon Msuva mwenye mabao 17.
Straika huyo wa zamani wa Vital ‘O ya Burundi, alisema kwenye kikosi cha Yanga ana wachezaji wengi wa kumchezesha na kumtengenezea nafasi za kufunga tofauti na ilivyokuwa akiwa Simba.
“Hilo lipo wazi, kama ningeanza msimu na Yanga ningemaliza mfungaji bora, nimecheza mechi chache na nimefunga mabao mengi, kama zile mechi saba za mwanzo ningekuwa Yanga ingekuwa balaa,” alisema.
“Hapa Yanga nina watu wengi wa kunitengenezea nafasi, kuanzia viungo hadi mawinga, hii ni tofauti na Simba ambapo watu wa kazi hiyo walikuwa wachache.”
0 comments :