Wachezaji wa timu ya Taifa wakifanya mazoezi kwenye uwanja wa CCM Kirumba,Mwanza kujiaandaa na mechi ya kirafiki dhidi ya Malawi keshokutwa jumapili.
MASHUTI ya washambuliaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa
Stars’ yaliyopigwa juzi Jumatano kwenye mazoezi ya timu hiyo
yanayoendelea katika Uwanja wa CCM Kirumba yamewapagawisha mashabiki wa
wa soka wa jijini hapa.
Mashabiki hao waliofika uwanjani hapo walijikuta
wakisema wazi kwamba kama mashuti hayo yatatumika kwenye pambano la
Jumapili dhidi ya Malawi, basi Stars itashinda mabao mengi.
Taifa Stars inafanya mazoezi jijini hapa na juzi
Jumatano walitumia muda mwingi kupiga mashuti langoni na kuwafanya
makipa Aishi Manula na Mwadin Ally kuipata freshi.
Mastraika Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu, John
Bocco walikuwa mwiba mkali kwa makipa hao kutokana na mashuti makali
yaliyokuwa yakilenga goli huku makipa hao wakijitahidi kuyapangua.
0 comments :