Ikitoka nytuma ya goli 1-0, Brazil iliisambaratisha Ufaransa kwa mabao 3-1 katika mchezo wa
kimataifa wa Kirafiki uliopigwa usiku wa jana Alhamis katika dimba la Stade de France.
Kiungo mshambulizi, Oscar alifunga goli la kusawazisha katika dakika ya 40 baada ya mlinzi wa Ufaransa, Raphael Varane kutangulia kuwafungia wenyeji katika dakika ya 21. Neymar alifunga goli la pili dakika ya 57, kisha kiungo, Luiz Gustavo akikamilisha hesabu baada ya kufunga bao la mwisho dakika ya 69.
Mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, kocha wa Brazil, Carlos Dunga amesema kuwa ataendelea kuwekeza mbinu zake ili kuifanya timu hiyo isipoteze uchezaji wake wa kawaida ‘ Samba’-Mchezo wa kupasiana huku wakimiliki mpira na kuutawanya kila pembe ya uwanja.
Ufaransa ilijitahidi kumiliki mpira na kuibana Brazil.
Timu zote zilimaliza dakika 0 zikiwa na asilimia 50-50 za umiliki wa mpira lakini vipaji zaidi vya Selecao ndivyo vilivyotoa tofauti kati ya ‘ Blues’ mabingwa wa dunia, 1998 na washindi hao mara tano wa Kihistoria ambao walifanya vibaya katika michuano iliyopita ya Kombe la dunia iliyopigwa Brazil- Brazuca 2014.
Neymar ndiye aliye chachu ya kikosi cha Dunga hivi sasa, akiwa amefunga mabao nane katika michezo ya hivi karibuni, mchezaji huyo hupiga mashuti golini mara kwa mara. Tofauti na alivyokuwa akicheza wakati wa utawala wa Big Phill, Dunga amefanya mabadiliko makubwa katika kutoka timu ambayo ilichapwa mabao 7-1 na Ujerumani katika nusu fainali ya kombe la dunia miezi tisa iliyopita.
0 comments :