Nathan mwenye umri wa miaka 19 atatua rasmi Stamford Bridge Julai 1 baada ya mkataba kati ya klabu hizo mbili kukubaliana.
Nathan alisema 'Nina furaha sana kujiunga na Chelsea, mabingwa wapya wa England, na nina matumaini nitakuwa na uwezo wa kujifunza mengi na kuendeleza mchezo wangu.
Kusainiwa kwa kiungo huyo kunaongeza safu ya Wabrazil katika klabu hiyo ya darajani, hivyo atajiunga na wakali kama Ramires, Willian, Oscar na Filipe Luis, wakati Blues pia kuwa vijana Wallace na Lucas.
Kiungo huyo alionyesha kiwango kizuri kwenye Kombe la Dunia la vijana Chini ya miaka 17 hapo ndipo Mapro wa Chelsea walipomwona.
Ingawa Brazil haikufika robo fainali ya mashindano hayo, Nathan alifunga mabao matano naalionyesha uwezo wake kamili.
Chelsea pia bado wanamwangalia kiungo Gerson, 17 kutoka Fluminense.
Kiungo Nathan alitanganza jina lake wakati wa michuano ya dunia ya vijana miaka miwili iliyopita yaliyofanyikia Abu Dhabi.
0 comments :