Ligi kuu ya Uingereza, EPL inatarajiwa kuanza tena siku ya Jumapili wakati ambapo mabingwa wa ligi hiyo Chelsea wanakutana na washindi wa Kombe la FA Arsenal katika Kombe la Charity Shield ( Ngao ya Hisani) itakayochezwa kwenye uwanja wa Wembley leo.
Mechi hiyo inajiri siku 64 baada ya kumalizika ligi hiyo ambapo Washika bunduki hao waliishinda Aston Villa 4-0 katika fainali ya FA.
Pande zote mbili hazijafanya usajili mkubwa katika msimu huu ijapokuwa kipa Petr Cech ataanzishwa dhidi ya timu yake ya zamani Chelsea.
Chelsea vilevile inaweza kumuanzisha mchezaji wao mpya Radamel Falcao iliyompata kwa mkopo akitokea klabu ya Manchester United.
Falcao mwenye umri wa miaka 29 aliichezea kilabu ya Manchester United msimu uliopita lakini hakuweza kutamba kwani aliweza kufunga mabao 4 tu katika mechi 29 alizocheza.
Leo hii timu hizo mbili zinakutana huku kocha wa Washika bunduki,Arsenal akitarajia kuishinda timu ya Chelsea kwa mara ya kwanza katika mechi 13 ilizozikutanisha timu hizo.
Makocha hao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakitofautiana kauli hali inayosababisha mechi ya leo kuwa kali na ya kusisimua.
Mourinho alisema kwamba Arsenal imetumia fedha nyingi msimu huu ikilinganishwa na Chelsea katika kipindi cha miaka kadhaa iliopita, huku Wenger akijibu kwamba hasikilizi kile watu wanachosema ama kufikiri.
0 comments :