Tangaza hapa

e

Featured Posts

Thursday, 23 July 2015

UEFA yaipiga faini klabu ya Barcelona

Unknown     22:34    


Shirikisho la mpira wa miguu Ulaya, UEFA limeipiga faini klabu ya Barcelona ya Hispania.

Hii imetokea baada ya mashabiki wa klabu hiyo kuonyesha mabango ya kisiasa katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyofanyika mwezi wa sita mwaka huu.

UEFA imeiamuru Barcelona kulipa faini ya Euro 30,000 ($ 33,000) kwa kosa hilo.

Mashabiki hao walionyesha mabango hayo kuhalalisha uhuru kwa kanda ya Catalonia ya Hispania katika Uwanja wa Olimpiki mjini Berlin.

Sheria za UEFA zinazuia masuala ya kisiasa, kidini, na kubeba mabango yoyote wakati wa mechi yoyote.

Klabu ya Barcelona ilifanikiwa kutwaa taji lake la tano musimu huu baada ya kuifunga Juventus  3-1 ambapo mechi hiyo ilifanyika tarehe 6 Juni mwaka huu katika katika uwanja wa Olimpiki mjini Berlin.

0 comments :

Top headlines

© 2011-2014 MICHEZONI. Designed by Alfred Meshack Bloggertheme9. Powered by Blogger.