Siku moja baada ya Real Madrid kutolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, uvumi umetanda juu ya Bale kuelekea Manchester United katika usajili wa majira ya kiangazi.
Nyota huyo wa zamani wa Tottenham amekuwa akicheza chini ya kiwango chake siku za hivi karibuni tangia ajiunge na klabu hiyo misimu miwili iliyopita.
Hivyo kampeni ya mchezaji huyo ghali kuelekea kwa Mashetani Wekundu ni kubwa kwani baadhi ya mastaa wake wako mbioni kutemwa na matajiri hao.
Star Sport imesema kuwa gharama ya uhamisho wa mchezaji huyo ni £ 80,000,000.
0 comments :