Tangaza hapa

e

Featured Posts

Saturday, 16 May 2015

EPL kuendelea wikiendi hii

Unknown     03:17    

Ligi Kuu ya Uingereza itaendelea tena wikiendi hii kwa nyasi za viwanja saba kuwaka moto katika siku ya jumamosi .

Southampton walioko katika nafasi ya 7 huku wakiwa wamejikusanyia alama 57 watakua wenyeji wa Aston Villa mchezo utakaofanyika katika uwanja wa St Mary's.

Burnley ambao tayari wameshuka daraja watakua katika uwanja wao wa nyumbani Turf Moor kuwakabili Stoke City.

Katika dimba la Loftus Road QPR watakua na kibarua cha kuwakabili Newcastle huku QPR wakikamilisha ratiba baada ya kuwa wameshashuka daraja tayari.

Sunderland atakua nyumbani Brittania kuwaalika Leicester City huku kila timu ikihitaji alama tatu kuweza kujinasua na janga la kushuka daraja.

Ligi hii itaendelea tena jumapili kwa michezo miwili kwa Swansea kucheza Man City huku Manchester United wakionyeshana ubavu na Arse.

0 comments :

Top headlines

© 2011-2014 MICHEZONI. Designed by Alfred Meshack Bloggertheme9. Powered by Blogger.