Tangaza hapa

e

Featured Posts

Saturday, 16 May 2015

Simba kusajili wachezaji kuziba pengo

Unknown     03:00    

Katika kile kinachoonekana ni kuweka mikakati ili kuchukua ubingwa msimu ujao, wekundu wa Msimbazi, Simba inahaha kutafuta wachezaji kutoka nje ya nchi ili kuimarisha kikosi chake.

Hatua hiyo inakuja baada ya Simba, iliyomaliza ya tatu katika msimu wa ligi iliyopita, kuripotiwa kuachana na wachezaji watatu wa kigeni kutoka Uganda, Simon Sserunkuma, Dan Sserunkuma na Joseph Owino kufuatia pendekezo la kocha Mserbia Goran Kopunovic.

Habari kutoka Simba zinasema sasa ni wakati wa kutafuta wachezaji katika nchi jirani za Afrika ili kuziba pengo la Waganda hao.

Baachi ya nchi ambazo zimeelezwa kuwa Simba inasaka wachezaji ni pamoja na Ghana, Nigeria, Rwanda, Burundi na Kenya.

Uamuzi huo unakuja baada ya Simba kuwe nje ya michuano ya kimataifa kwa takriban miaka mitatu mfululilizo.

Ligi kuu ya Tanzania Bara imekwisha hivi karibuni huku Yanga ikiwa bingwa na waliokuwa mabingwa watetezi, Azam kumaliza nafasi ya pili.

Yanga na Azam ndio wawakilishi wa Tanzania Bara katika michuano ya vilabu ya CAF hapo mwakani.

Yanga itashiriki kombe la Washindi barani Afrika na Azam itashiriki kombe la Shirikisho.

0 comments :

Top headlines

© 2011-2014 MICHEZONI. Designed by Alfred Meshack Bloggertheme9. Powered by Blogger.