Mshambuliaji wa Manchester United Robin van Persie amekubali kuondolewa Old Trafford baada ya kupitia magumu msimu huu.
Mshambuliaji huyo amebakiwa na mwaka mmoja tu wa kumaliza mkataba wake wa sasa.Van Persie ana matumaini ya kuendelea kucheza kwa miaka michache ijayo kabla ya kutundiga daluga.
Dante atakiwa Manchester United.
Dante ambaye ni mchezaji wa kimataifa kutoka Brazil, anatazamiwa kuisaidia timu hiyo kujenga ukuta imara ili kuweza kuleta mafanikio zaidi kwenye klabu hiyo yenye maskani yake jijini Manchester.
Lakini mchezaji mwenyewe, Dante ameonyesha bado ana furaha ya kutaka kuendelea kuitumikia timu yake ya Bayern Munich kwa misimu mingine zaidi.
Real Sociedad yakaribia kumsajili Joel Campbell kutoka Arsenal.
Klabu ya Real Sociedad ya Hispania ina matumaini kwamba itaweza kupata saini ya mshambuliaji Joel Campbell kutoka Arsenal.
Campbell ambaye alitumia nusu ya msimu uliopita akiwa Villarreal kwa mkopo, klabu yake ya Arsenal itaamua kumuuza mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Costa Rica kwenda klabu hiyo ya Real Sociedad kama makubaliano yakifikiwa baina ya pande hizo mbili.
Manchester United yaongoza mbio za kumng'oa Alves Camp Nou.
Manchester United wanaamini wapo sehemu nzuri kuweza kupata huduma ya beki Dani Alves kutoka Barcelona.
Kocha Louis van Gaal anataka kusaini beki wa kulia,beki mwingine anayetolewa macho na United ni beki wa Everton Séamus Coleman na Gregory van der wiel wa Paris Saint-Germain.
Monaco yavutiwa na huduma ya Mirallas.
Klabu ya Monaco ya Ufaransa imevutiwa na kiwango cha Kelvin Mirallas kutoka klabu ya Everton ya Uingeleza.
Mbeligji huyo aliwasili katika klabu hiyo ya Everton msimu wa 2012/2013 akitea klabu ya Olympiakos ya Ugiriki.
Inter-milan yavutiwa na Benatia.
Klabu ya Inter-milan ya Italia inataka kumrudisha beki wa kati Mehdi Benatia kutoka klabu ya Bayern Munich.
Beki huyo mzaliwa wa Ufaransa lakini huchezea timu ya taifa ya Morocco, kabla ya kusajiliwa Bayern Munich, alikuwa anakikipiga katika klabu ya AS roma ya Italia.
0 comments :