Tangaza hapa

e

Featured Posts

Wednesday, 3 June 2015

ANGALIA HAPA TETESI ZA USAJILI ZILIZOJILI HII LEO BARANI ULAYA.

Unknown     02:05    























Klabu ya Manchester United  iko katika nafasi nzuri ya kukamilisha usajili wa beki kutoka klabu ya  Barcelona iwapo kocha Louis Van Gaal atataka kumsajili beki huyo wa kulia kutoka Brazil.
Alves atakuwa hana mkataba mwishoni mwa msimu huu na Barcelona iko tayari kumwachilia beki huyo mwenye umri wa miaka 32 kuondoka baada ya mechi ya fainali ya klabu bingwa Ulaya dhidi ya Juventus siku ya jumamosi mjini Berlin.

Klabu ya PSG pia inamuwania Alvez ijapokuwa kocha wake Laurent Blanc anaamini mchezaji huyo bado anataka kusalia Barcelona.
Lakini maoni ya Old Trafford ni kwamba Alvez hangependelea kujiunga na PSG

Van Gaal anapanga kumsajili beki wa kulia.Licha ya umri wake mkubwa ukosefu wa fedha za uhamisho zinamfanya mchezaji huyo kuwa muhimu.

Mchezaji huyo wa Brazil anapokea kitita cha pauni 120,000 kwa wiki, fedha ambazo United inaweza kuzilipa bila kutoa jasho.

Falcao kuelekea Chelsea.

Radamel Falcao applauds fans as he is substituted

Mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza, Chelsea, wanadaiwa kuwa katika mazungumzo na mshambuliaji mkolombia Radamel Falcao.

Mchezaji huyo yupo AS Monaco kwa sasa baada ya kuichezea Manchester United kwa mkopo wa muda mrefu ambao wamekataa kumpa mkataba wa moja kwa moja.

Hata hivyo kulingana na Sky Sports, Chelsea ni miongoni mwa vilabu vilivyo katika mazungumzo na mshambuliaji huyo ambae hakua katika kiwango chake msimu huu alipokua na mashetani wekundu.

Falcao, mwenye miaka 29,  alifanikiwa kufunga magoli manne pekee katika michezo 29 aliyocheza Premier League.

Kuondoka kwa Didier Drogba Chelsea, kumemuacha Mourinho na machaguo ya washambuliaji wawili tu, Diego Costa na Loic Remmy, hivyo Falcao anaonekana kuhitajika kwa kiasi kikubwa.

Hata hivyo Sky Sports wanadai mshahara mkubwa anaohitaji Falcao unaweza kua kikwazo cha mkolombia huyo kutua darajani.

 Arsenal kumsainisha Jackson Martinez Arsenal Transfer News: Latest on Jackson Martinez and Gonzalo Higuain Rumours

Mshambuliaji huyo wa Porto anadaiwa kuwa katika mpango wa kusaini The Gunners.

Inadaiwa klabu hiyo iliyoko kaskazini mwa London imemtengea kiasi cha pauni 24.7 na muda tu ndio unaosubiriwa mchezaji huyo kusaini.

Manchester United kumvuta Bacca


Mashetani wekundu wanapewa nafasi kubwa zaidi ya kuipata saini ya mshambuliaji wa Sevilla, Carlos Bacca.

 Mchezaji huyo aliyefunga magoli mawili katika fainali za Europa anaonekana kua na uelekeo mkubwa wa kucheza EPL lakini itawagharimu Man U kiasi kisichopungua pauni mil. 21.3

AS Roma wanamfukuzia Dzeko
Liverpool Transfer News: Latest on Edin Dzeko and Mateo Kovacic Rumours

Mshambuliaji wa Manchester City ameonekana kuwavutia zaidi waitaliano AS Roma, hata hivyo msimu huu hakua katika kiwango chake, hali inayowarahisishia Roma kumpata kwa urahisi zaidi.

Khedira kuelekea Juventus

Khedira on verge of Juventus move - Marotta

Mchezaji anayeonekana kutopewa nafasi sana klabuni Real Madrid anaweza kutimkia Juve.

Kulingana na ripoti, tayari Juve wameshatumiwa ripoti ya afya ya Khedira, na anaonekana yuko fiti.
Kinachotakiwa tu kwa sasa ni Juve nao kufanya vipimo vyao.

Man United wakanusha kuhusu  Gundogan
Ilkay Gündogan

Manchester United wamekanusha ripoti kuwa wana mpango wa kumsajili kiungo wa Borussia Dortmund Ilkay Gundogan.

Hata hivyo mkurugenzi wa Borussia Hans-Joachim Watzke ameshatangaza kumfungulia milango mchezaji huyo, lakini mpaka sasa haijaeleweka ni wapi ataelekea.

0 comments :

Top headlines

© 2011-2014 MICHEZONI. Designed by Alfred Meshack Bloggertheme9. Powered by Blogger.