Mkufunzi wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho ametangazwa kuwa mkufunzi bora katika ligi kuu ya Uingereza kwa mara ya tatu.
Akihudumia
kipindi chake cha pili katika klabu hiyo, meneja huyo mwenye maneno mengi kutoka Ureno (52) aliiongoza Chelsea kubeba taji lao la kwanza la ligi ya
Uingereza katika kipindi cha miaka mitano pamoja na kombe la Ligi.
Kiungo wa Chelsea Eden Hazard ambaye aliifungia Chelsea mabao 20
alitangazwa kuwa mchezaji bora wa ligi hiyo ya Uingereza msimu huu.
0 comments :