Tangaza hapa

e

Featured Posts

Thursday, 21 May 2015

Coutinho achaguliwa mchezaji bora wa msimu wa Liverpool

Unknown     02:25    

Philippe Coutinho amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka kwa msimu huu katika klabu ya Liverpool jana Jumanne.
 
Coutinho (22), amefunga magoli matano na kutoa pasi tano za magoli katika michezo 34 ya ligi aliyocheza msimu huu, huku akiwashinda Rahim Sterling, Martin Skrtel, Jordan Henderson na Simon Mignolet katika tuzo hiyo.

Kiungo huyo amekuwa kwenye kiwango kizuri tangu ajiunge na klabu hiyo akitokea klabu ya Inter Milan ya Italia.
 
“Hiki ni kitu maalumu sana kwangu, pia ina maana kubwa sana kuipokea kutoka kwa Gerrard, sina zaidi cha kuongeza bali ninatoa shukrani zangu za dhati kwa wachezaji wenzangu wote kwa mchango wao,” alisema kiungo huyo mahiri kutoka Brazil. 
 
 
 
 

0 comments :

Top headlines

© 2011-2014 MICHEZONI. Designed by Alfred Meshack Bloggertheme9. Powered by Blogger.