MANCHESTER United wanatarajia kuipa Arsenal kipigo cha pili msimu huu wanapokutana leo katika mechi ya ligi kuu England uwanja wa Old Trafford.
Louis van Gaal alishinda 2-1dhidi ya Arsenal katika uwanja
wa Emirates mwezi Novemba mwaka jana na leo anahitaji kushinda kwa mara ya pili msimu huu.
Baada
ya kupoteza mechi tatu mfululizo, United walishinda
dhidi ya Crystal Palace wiki iliyopita na kimahesabu wanahitaji pointi
moja tu
kufuzu ligi ya mabingwa Ulaya msimu ujao, ingawa Liverpool wanaoshika
nafasi ya tano wapo nyuma kwa pointi sita, ambao wana wastani mbaya wa magoli
ya kufunga na
kufungwa.
Gunners ambao walishinda 2-1 dhidi ya Man United Old
Trafford katika mechi ya raundi ya sita ya kombe la FA, leo wanahitaji kushinda
ili kuipiku Man City kushika nafasi ya pili msimu huu.
HABARI ZA TIMU
Wayne Rooney na Luke Shaw wanaikosa mechi ya leo kutokana na
majeruhi waliyopata wiki iliyopita kwenye mechi dhidi ya Crystal Palace.
Marcos Rojo, Angel Di Maria na Robin van Persie wako
hatarini kuikosa mechi hii wakati Michael Carrick na Rafael wako nje kwa mechi zote
za ligi kuu zilizosalia.
Danny Welbeck anakosa nafasi ya kucheza dhidi ya timu yake
ya zamani kwasababu ya majeruhi ya goti na Mathieu Debuchy hayupo pia.
TAKWIMU MUHIMU
Manchester United hawajawahi kufungwa katika mechi 7 za
nyumbani dhidi ya Arsenal (Wameshinda 6, sare 1) tangu walipofungwa 1-0 mwezi
septemba 2006.
Wayne Rooney amefunga magoli 11 dhidi ya Arsenal katika
mechi za ligi kuu England, lakini amefunga magoli mengi zaidi dhidi ya Aston Villa
(13) na Newcastel (12).
United hawajaruhusu kufungwa zaidi ya goli moja katika
uwanja wa nyumbani dhidi ya Arsenal na kupoteza mechi ya ligi tangu februari
1979.
Arsenal inaweza kuwa timu ya nne kihistoria kuifunga Man
United mara mbili Old Trafford katika msimu huo huo.
Timu nyingine zilizowahi
kufanya hivi ni Chelsea (2004/2005), Tottenham (1989/90) na Aston Villa (1919/20).
Manchester United wameshindwa kuzuia kufungwa goli katika
mechi saba walizocheza na mara ya mwisho kucheza mechi 8 bila kuruhusu nyavu
zao kuguswa ilikuwa septemba 2001.
0 comments :