Kiungo wa Chelsea, Cesc Fabregas amechaguliwa kuwa ndie kiungo bora katika ligi zote barani Ulaya akiwashinda Paul Pogba, Sergio Busquets na Xabi Alonso.
Kiungo huyo alipata alama 100 kati ya wachezaji wote aliokuwa anashindana nao.
Vitu vya msingi vilivyozingatiwa katika utoaji wa tuzo hiyo ni pamoja na uwezo wa kutoa pasi za mwisho za magoli,kupanda na kushuka ili kuisaidia timu icheze ,kuchukua na kusambaza mpira.
Mchuano huo ulihusisha viungo wote wanaocheza katika ligi kuu tano za Ulaya.
Kiungo wa Paris Saint-Germain,Marco Verratti alichukua nafasi ya pili kwa alama 96.3, wakati kiungo wa Bayern Munich Xabi Alonso alishika nafasi ya tatu.
0 comments :