Mshambuliaji timu ya soka ya Yanga, Simon Msuva, amefanikiwa kuzoa tuzo mbili kutokana na jinsi alivyoisaidia timu yake kupata ubingwa wa Ligi kuu ya Vodacom.
Msuva
ambaye aliibuka kinara wa mabao kwenye safu ya ufungaji bora baada ya kufunga
jumla ya magoli 17 kwenye msimu uliomalizika Mei 9 mwaka huu pia mchezaji huyo alipata tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa VPL.
kutokana na Msuva kuwa
kwenye majukumu ya timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, zawadi zake
zilichukuliwa na wawakilishi wake ambaye ni baba yake mzee Msuva aliyeambana na mkewe mama yake Simon Msuva.
Msuva amewabwaga Mrisho Ngassa na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ kwenye kinyang’anyiro hicho cha mchezaji bora wa ligi.
Nafasi nyingine ambazo zilikuwa
zikiwaniwa ni pamoja na mlinda mlango bora ambapo tuzo hiyo imenyakuliwa
na Shaban Kado (Coastal union) ambaye kwa sasa amesaini kuitumikia
klabu ya Mwadui FC ya Shinyanga akiwabwaga Mohamed Yusuph (Tanzania
Prisons) na Said Mohamed (Mtibwa Sugar).
Wengine waliotwaa tuzo mbalimbali ni hawa hapa:
Kocha bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015 ilikwenda kwa Mbwana Makata ambaye ni mkufunzi watimu ya Tanzania Prisons akiwashinda Goran Kopunovic (Simba SC) na Hans Van Der Pluijm (Young Africans)
Mwamuzi bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015 ilikwenda kwa Israel Mjuni Nkongo akiwashinda Jonesia Rukyaa pamoja na Samwel Mpenzu.
Timu yenye nidhamu Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015 ilichukuliwa na timu ya Mtibwa Sugar ikizishinda timu za Mgambo JKT na Simba SC.

0 comments :