Mshambuliaji nyota wa TP Mazembe, Mbwana Samatta ameshambuliwa kwa mawe na mashabiki wa timu ya Shark.
Mbwana raia wa Tanzania anayefanya vizuri nchini DR Congo, amesema ameshangazwa na mashabiki wale kuingia na mawe uwanjani.
"Wamenijeruhi, nilihisi kitu kimenipiga kichwani. Nilivyoshika hivi kuangalia mkononi, damu. Nikajua nimeumia.
"Nimepatiwa matibabu,
ninaendelea vizuri kabisa. Lakini hawa jamaa walikuwa na mawe mengi
kabisa pale uwanjani," alisema Mbwana alipozungumza moja kwa moja na
SALEHJEMBE kutoka Lubumbashi, DR Congo.
"Unajua mechi ilikuwa si
nzuri kwetu. Jamaa walituotea fasta na kutufunga mbili. Baada ya hapo
tutakaanza kupambana lakini tulifanikiwa kupata bao moja. Mwisho ikawa
2-1.
"Mechi imeisha, fujo zikaanza, wakaanza kurusha mawe na mwisho ndiyo ikawa hivyo."
Mshambuliaji huyo Mtanzania ni tegemeo la safu ya ushambulizi ya TP Mazembe.
Kwa hisani ya Saleh Jembe
0 comments :