Kocha wa Arsenal, Mfaransa Arsene
Wenger ameshangazwa na namna chama cha soka England, FA kilivyopanga
ratiba ambapo mechi kubwa ya ligi kuu kati ya Chelsea na Manchester
United itayochezwa keshokutwa itatofautiana kwa dakika kumi na mechi ya
nusu fainali ya kombe la FA.
Reading na Arsenal zitachuana
katika mechi ya nusu fainali ya kombe la FA jumamosi majira ya saa moja
dakika ishirini kwa saa za Africa mashariki na dakika kumi baadaye
itaanza mechi kubwa ya ligi kuu baina ya Chelsea na Manchester United
uwanja wa Stamford Bridge.
Wenger amesema mechi ya ligi kuu
ni kubwa kwa Chelsea na kama watapoteza mbio za ubingwa zitakuwa wazi,
lakini wangependa kuona mechi yao inakuwa ya kipekee kwasababu ni nusu
fainali, hivyo isingeingiliana na mashindano mengine.
Wakati huo huo Mfaransa huyo
amekanusha taarifa za Jurgen Klopp kuchukua nafasi yake Emirates akidai
ni uzushi unaopaswa kupuuzwa kwani bado ana mipango na timu yake.
0 comments :