Tangaza hapa

e

Featured Posts

Saturday, 30 May 2015

Mgosi asaini tena Msimbazi.

Unknown     04:32    
 
Mshambuliaji wa Mtibwa sugar, Musa Hassan 'Mgosi' amezifunga Simba, Yanga na Azam kwenye msimu uliopita.

Jumanne ya wiki hii, Mgosi alisaini mkataba wa kazi na klabu yake ya zamani ya Simba baada ya mkataba wake na Mtibwa kumalizika.

Hata hivyo, Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) bado halijafungua rasmi usajili kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na ndio maana klabu zote nyingi zinawasainisha mikataba wachezaji wapya, huwa wanawapa mikataba ya kazi ambayo ni ya klabu na baadaye watasaini mikataba inayotambulika na TFF.

Chanzo cha habari kutoka Simba, kilisema kuwa Mgosi alisaini mkataba huo baada ya kufikia makubaliano na viongozi na hivyo atatangazwa rasmi pindi dirisha la usajili litakapofunguliwa.

Kwa upande wa Mgosi wakati akihojiwa na chanzo hiki alisema: “Kilichofanyika ni mazungumzo tu ya usajili ambayo yamefikia pazuri, kama tutafikia makubaliano basi nitasaini na nitacheza Simba msimu ujao, hivyo ngoja tusubiri.”

Mpaka sasa Simba imemsajili mchezaji kutoka Mbeya City FC, Peter Malyanzi na kuwaongeza mikataba mipya wachezaji wake wa zamani Said Ndemla, Hassan Isihaka, Ibrahim Ajibu huku wengine kama William Lucian ‘Gallas’ na Abdallah Seseme pamoja na Ramadhan Singano wakiwa katika mazungumzo ya kuongezewa mikataba mipya.

YANGA YAMPELEKA KASEKE TAIFA STARS

Unknown     04:00    

 Taarifa iliyoporipotiwa na Saleh Ally inasema kwamba kiungo mpya wa Yanga, Deus Kaseke ameongezwa katika kikosi cha timu ya taifa kinachojiandaa kuivaa Misri.

Kaseke ambaye amesajiliwa na Yanga siku chache zilizopita kwa dau la Sh milioni 35 akitokea Mbeya City FC,yuko pamoja na wachezaji wengine watatu walioongezwa katika kikosi hicho.

Wachezaji hao wote wameanza mazoezi leo kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.
 
Wengine walioongezwa katika kikosi hicho ni kipa wa Mtibwa Sugar, Said Mohammed 'Nduda" pia beki wa timu hiyo Andrew Vincent na kiungo wa Azam FC, Gardiel Michael.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij ambaye amekalia kuti kavu kutokana na kikosi chake kwenda mwendo wa kusua, ameamua kuimarisha kikosi chake na imeelezwa atafanya mchujo kabla ya kwenda Misri.

Top headlines

© 2011-2014 MICHEZONI. Designed by Alfred Meshack Bloggertheme9. Powered by Blogger.