Kiungo wa Simba SC na timu ya Taifa ya Tanzania, Jonas
Mkude leo anakwea ‘pipa’ kuelekea Afrika Kusini kwenda kufanya
majaribio kwenye klabu ya Wits University inayoshiriki ligi kuu ya
nchini humo.
Wakati kiungo huyo akielekea bondeni, wachezaji walioitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ wanakutana leo kwenye hotel yaTansoma
kuzungumza na kocha wao mpya.
Afisa habari wa klabu ya Simba, Hajji Manara amesema kwamba Simba wamempa barakazote kiungo huyo licha ya kuwa ameitwa kwenye timu ya Taifa.
Afisa habari wa klabu ya Simba, Hajji Manara amesema kwamba Simba wamempa barakazote kiungo huyo licha ya kuwa ameitwa kwenye timu ya Taifa.
Manara
amesema tayari wamezungumza na kocha wa Stars, Boniface Mkwasa kumpa taarifa
hiyo ya kiungo wao anaekwenda kufanya majaribio ya siku 14 (wiki mbili).
“Tumempa
baraka zote za kwenda kufanya ‘trial’ lakini kumalizana naye ni mpaka hapo
baadae atakapofuzu lakini tumempa baraka zote ‘full’, amepata ‘support’ ya
Simba”, alisema Manara.
“Ni
kweli Mkude ameitwa kwenye timu ya Taifa lakini Mungu jaalia tumeshazungumza na
Mwalimu Charles Boniface Mkwasa na kumpa taarifa hiyo kwamba Jonas anaondoka na
yeye alikuwa hana taarifa hiyo lakini nadhani haitakuwa tatizo kwake kwasababu
anachoenda kukifanya pia ni nsehemu ya ‘program’ za TFF, lazima tuongeze
‘professionals’ wengi zaidi nadhani ni baraka kwa nchi, Boniface hatakuwa na
shida, ni mwalimu mweledi sana”, ameeleza.
“Anakwenda
Wits University jina lao la utani wanaitwa ‘The clever boys’ ilishika nafasi ya
tatu kwenye msimu uliopita, atafanya majaribio ya siku 14 pale”,
alimaliza Manara.
Kiungo huyo ataungana na wachezaji wengine wa Tanzania waliowahi kufanya majaribio katika ligi hiyo ya Afrika Kusini kwa siku za hivi karibuni kama Mrisho Ngassa na Simon Msuva. Ambapo ni Ngassa tu ndiye aliyefuzu kucheza katika ligi hiyo.
0 comments :