Tangaza hapa

e

Featured Posts

Thursday, 23 July 2015

UEFA yaipiga faini klabu ya Barcelona

Unknown     22:34    

Shirikisho la mpira wa miguu Ulaya, UEFA limeipiga faini klabu ya Barcelona ya Hispania.

Hii imetokea baada ya mashabiki wa klabu hiyo kuonyesha mabango ya kisiasa katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyofanyika mwezi wa sita mwaka huu.

UEFA imeiamuru Barcelona kulipa faini ya Euro 30,000 ($ 33,000) kwa kosa hilo.

Mashabiki hao walionyesha mabango hayo kuhalalisha uhuru kwa kanda ya Catalonia ya Hispania katika Uwanja wa Olimpiki mjini Berlin.

Sheria za UEFA zinazuia masuala ya kisiasa, kidini, na kubeba mabango yoyote wakati wa mechi yoyote.

Klabu ya Barcelona ilifanikiwa kutwaa taji lake la tano musimu huu baada ya kuifunga Juventus  3-1 ambapo mechi hiyo ilifanyika tarehe 6 Juni mwaka huu katika katika uwanja wa Olimpiki mjini Berlin.

Wednesday, 22 July 2015

News... TFF yabadili ratiba ya kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara, sababu ni hii hapa ...

Unknown     05:28    












Shirikisho la la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limetangaza kubadili tarehe ya kuanza kwa Ligi Kuu ya Soka Tanzania bara (VPL).
Shirikisho hilo limefanya uamuzi huo kutokana na kubadilishwa kwa kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars jukumu ambalo alipewa Charles Boniface Mkwasa.
Ligi kuu Tanzania ilikuwa ianze august 22 2015 lakini kwa sasa itaanza Septemba12 2015 kwa lengo la kumpa kocha huyo muda wa kutosha kukinoa kikosi hicho cha Taifa ambacho kitacheza na Timu ya Taifa ya Nigeria Septemba 5 mwaka huu.
download
Ambapo mchezo wa Ngao ya Jamii utakaozikutanisha timu za Yanga na Azam FC utachezwa August 22 badala ya August 15 iliyokuwa imepangwa awali.
Ratiba ya Ligi kuu sasa inafanyiwa marekebisho na mechizitakuwa zinachezwa katikati ya wiki na siku za weekend isipokuwa Oktoba 25 2015 ambapo hakutakuwa na mchezo wowote ilikupisha Uchaguzi Mkuu wa Raisi na Wabunge wa Tanzania.
Boniface-Wambura1-2
Klabu zinazoshiriki Ligi hiyo zimeandikiwa barua kupewa taarifa hiyo na wamiliki wa viwanja wameandikiwa barua kukarabati viwanja hivyo ili viweze kukidhi vigezo vya kutumika katika michezo ya Ligi kuu na Ligi Daraja la Kwanza vininevyo havitaruhusiwa kutumika. 

Top headlines

© 2011-2014 MICHEZONI. Designed by Alfred Meshack Bloggertheme9. Powered by Blogger.