Tangaza hapa

e

Featured Posts

Monday, 8 June 2015

Kauli ya David De Gea kuhusu Manchester United na Real Madrid.

Unknown     18:31    
Habari ambazo mashabiki wa Manchester United wamekuwa wakihofia kuzipata hivi karibuni hatimaye zimekuwa kweli baada ya kipa namba moja wa klabu iyo Mhispania David De Gea kuiambia klabu hiyo kuwa anataka kuhamia Real Madrid .

De Gea kupitia wakala wake ameiarifu United kuwa dhamira yake ni kujiunga na Madrid na amefikia uamuzi huo baada ya kipindi kirefu cha kuwaza na kuamua ni hatua ipi bora ya kufuata kwenye mustakabali wake .

De Gea amekaa na United kwa muda wa miaka minne tangu aliposajiliwa toka Atletico Madrid kwa ada ya uhamisho ambayo iliweka rekodi kwa makipa ya paundi milioni 17 na amekaa United kwa muda wa miaka minne , muda ambao amepitia hatua kubwa kiasi cha kufikia kuwa na kiwango cha ubora wa dunia .

Hivi karibuni De Gea alipewa ofa ya kuongezewa mshahara mpaka kufikia paundi 200,000 kwa wiki ofa ambayo hajaikubali akiwa amefikia uamuzi wa kurudi nyumbani kwao kwenye mji aliozaliwa na kukulia huku akipata fursa ya kuwa karibu na mpenzi wake Edurne .

De Gea amekuwa kwenye mipango ya Real Madrid kwa muda mrefu ambapo klabu hiyo imemuweka kama chaguo namba moja la kuziba nafasi ya mkongwe Iker Casillas ambaye umri wake unazidi kuwa mkubwa .

Endapo usajili huu wa David De Gea kuondoka United na kuhamia Hispania kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu , kipa huyo atakuwa mchezaji wa tano kuondoka United baada ya Cristiano Ronaldo , David Beckham , Ruud Van Nistelrooy na Gabriel Heinze.

Sunday, 7 June 2015

Xavi atabiri nani atakua mkali wa dunia baada ya Messi.

Unknown     17:05    


Kiungo mkongwe wa Barcelona, Xavi Hernandez amefunguka kua ni nani ataekaliakiti cha Messi ikitokea Messi anastaafu.
Mkali huyo anaamini Mbrazil, Neymar ndiye atakaekua mchezaji bora wa dunia kwa miaka ijayo.

Ana kipaji, Leo Messi akistaafu atakua naamini atakua mchezaji bora bila shaka" aliiambia UEFA.com.

Anafanya makubwa akiwa na umri wa miaka 23 pekee, na kufanya hivyo ukiwa Barcelona si mchezo.

Neymar anaenda kua na wakati mzuri, hafanyi makosa.

Xavi pia alisema kua Neymar ni mtu poa sana japo huripotiwa vibaya na baadhi ya wapinzani wake.

Neymar amefunga magoli 39 na kutoa usaidizi mara 11 katika michezo 51 na wakali hao wa Catalan.

Top headlines

© 2011-2014 MICHEZONI. Designed by Alfred Meshack Bloggertheme9. Powered by Blogger.