Tangaza hapa

e

Featured Posts

Sunday, 7 June 2015

Angalia hapa tetesi za usajili zilizojili hii leo kwenye magazeti ya Ulaya.

Unknown     15:04    


Real Madrid inataka kumuuza mshambuliaji wake Karim Benzema mwenye umri wa miaka 27 kwenda Manchester United katika jitihada za kuongeza kasi ya kupata saini ya kipa David De Gea mwenye umri wa miaka 24. (AS English)

Tottenham imejiunga katika mbio za kuwania saini ya mshambuliaji wa Aston Villa, Christian Benteke kwa ada ya £ 20m.
Lakini kwenye mkataba wake kuna kifungu kinachodai kwamba mchezaji huyo ataweza kuuzwa kwa £ 32.5m kama timu yoyote ikimhitaji.
Mshambuliaji huyo pia anawindwa na klabu za Liverpool na Chelsea zote za England  (The Sun)

Manchester City wanaangalia uwezekano wa kuanza harakati za kumfuatilia kiungo wa Bayer Leverkusen, Lars Bender, 27 kama itashindwa kupata saini ya kiungo wa Juventus, Paul Pogba(Mirror).

Arsenal imeongeza kasi ya kuhitaji saini ya mshambuliaji kutoka Colombia, Jackson Martinez,28  kwa dau la £ 25.7m baada ya Porto kukataa ofa kutoka Atletico Madrid (Metro).

Timu iliyopanda daraja ya Norwich City inawania saini ya winga wa Hull City, Robbie Brady, 23. (Hull Daily Mail)

Meneja wa Crystal Palace, Alan Pardew anataka kuwasajili Loic Remy kutoka Chelsea na Yohan Cabaye kutoka PSG.  (Daily Express)









Barcelona yatwaa kombe la UEFA kwa mara ya tano ikiiua Juve mjini Berlin Ujerumani.

Unknown     01:30    

Timu ya soka ya Barcelona kutoka Hispania imefanikiwa kutwaa kombe la tano la Uefa Champions League baada ya kuifunga timu ya Juventus mabao 3-1.

Wachezaji wa Barcelona kama kawaida yao walianza mchezo kwa kasi huku wakigongeana pasi za uhakika na katika dakika ya nne, Ivan Rakitic aliandika bao la kwanza akimalizia pasi murua ya kiungo fundi, Andres Iniesta.
 
Bao hilo lilidumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.
Kipindi cha pili Juventus waliimarika na kusawazisha goli hilo kupitia kwa Alvaro Morata aliyemalizia mpira uliotemwa na golikipa wa Barcelona kutokana na shuti kali la Carlos Tevez.

Dakika ya 68' Lionel Messi alipiga shuti kali lililotemwa na kipa wa Juve, Buffon na mpira kumkuta Luis Suarez aliyefunga goli ta pili na la ushindi.
 
 Dakika za nyongeza, Neymar akaifungia Barcelona goli la tatu kutokana na shambulizi la kushitukiza.

 
Barcelona ambayo iko chini ya Luis Enrique wamefanikiwa kutwaa makombe matatu msimu huu kwani awali walitwaa La Liga na kombe la Mfalme 'Copa del Rey'.







 

Top headlines

© 2011-2014 MICHEZONI. Designed by Alfred Meshack Bloggertheme9. Powered by Blogger.