Beki kisiki wa Arsenal Shkodran Mustafi anatarajiwa kuihama klabu yake hiyo. Hiyo imeripotiwa baada ya vilabu vya Inter Milan na Juventus zote za Italia kuonyesha kumhitaji mchezaji huyo raia wa Ujerumani.
Mchezaji huyo alijiunga na Arsenal kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 35 akitokea klabu ya Valencia ya Hispania na Arsenal wanataka kumuuza kabla ya dirisha kubwa la usajili halijafungwa.
Source: Dailymail
Pia kiungo wa Arsenal Alex Oxlade Chamberlain anatarajiwa kuondoka klabuni hapo baada ya timu hiyo kuhofia kumpoteza bure msimu ujao ambapo mkataba wake utakuwa umeisha.