Tangaza hapa

e

Featured Posts

Wednesday, 22 July 2015

News... TFF yabadili ratiba ya kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara, sababu ni hii hapa ...

Unknown     05:28    












Shirikisho la la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limetangaza kubadili tarehe ya kuanza kwa Ligi Kuu ya Soka Tanzania bara (VPL).
Shirikisho hilo limefanya uamuzi huo kutokana na kubadilishwa kwa kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars jukumu ambalo alipewa Charles Boniface Mkwasa.
Ligi kuu Tanzania ilikuwa ianze august 22 2015 lakini kwa sasa itaanza Septemba12 2015 kwa lengo la kumpa kocha huyo muda wa kutosha kukinoa kikosi hicho cha Taifa ambacho kitacheza na Timu ya Taifa ya Nigeria Septemba 5 mwaka huu.
download
Ambapo mchezo wa Ngao ya Jamii utakaozikutanisha timu za Yanga na Azam FC utachezwa August 22 badala ya August 15 iliyokuwa imepangwa awali.
Ratiba ya Ligi kuu sasa inafanyiwa marekebisho na mechizitakuwa zinachezwa katikati ya wiki na siku za weekend isipokuwa Oktoba 25 2015 ambapo hakutakuwa na mchezo wowote ilikupisha Uchaguzi Mkuu wa Raisi na Wabunge wa Tanzania.
Boniface-Wambura1-2
Klabu zinazoshiriki Ligi hiyo zimeandikiwa barua kupewa taarifa hiyo na wamiliki wa viwanja wameandikiwa barua kukarabati viwanja hivyo ili viweze kukidhi vigezo vya kutumika katika michezo ya Ligi kuu na Ligi Daraja la Kwanza vininevyo havitaruhusiwa kutumika. 

Monday, 20 July 2015

Messi azindua uwanja wa Gabon utakaotumika kuandaa mechi za fainali za kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2017.

Unknown     22:36    

 Mshindi wa tuzo ya mchezaji bora duniani mara nne ,Lionel Messi, amekutana na rais wa Gabon Ali Bongo Ondimba.
Mchezaji wa Argentina na mabingwa wa ligi kuu ya Ulaya Barcelona aliweka jiwe la msingi la uwanja utakaotumika kuandaa mechi za fainali za kombe la Mataifa ya Afrika mwaka wa 2017.
Mchezaji huyo maarufu wa klabu ya Barcelona ya Hispania alizindua rasmi mchakato wa ujenzi katika uwanja wa soka wa Port-Gentil.
Sherehe za uzinduzi huo zilifanyika kwenye eneo kubwa la mchanga ambapo uwanja huo wa soka utajengwa.
Ni ziara ya kwanza ya mshambuliaji huyo wa Argentina nchini Gabon na aliweka saini yake kwenye jezi zinazovaliwa na mashabiki wake , kabla ya kuweka jiwe la msingi akiambatana na rais.

null
Uwanja huo mpya utakua na uwezo wa kuwapokea mashabiki 20,000

" Nilipokua Barcelona miaka michache iliyopita , nilikutana na Messi ambaye aliniambia kwamba atakuja kunitembelea mjini Libreville," alisema rais wa Gabon.
" Ni ahadi aliyonipa.''
''Ni mtu anayetimiza ahadi ."
Uwanja huo mpya utakua na uwezo wa kuwapokea mashabiki 20,000 na unatarajiwa kuandaa mechi kuanzia mwezi Novemba 2016 katika michezo ya awali ya shindano hilo.

Top headlines

© 2011-2014 MICHEZONI. Designed by Alfred Meshack Bloggertheme9. Powered by Blogger.