Tangaza hapa

e

Featured Posts

Monday, 10 August 2015

Mwandishi wa makala za michezo apigwa hadi kufa na mashabiki.

Unknown     20:29    

Mwandishi wa habari za michezo amepigwa hadi kufa na mashabiki wa mchezaji aliyemkosoa katika ripoti yake.

Rasim Aliyev raia wa Azerbaijan alimkashifu mchezaji nyota wa klabu ya Gabala ;Javid Huseynov, katika mtandao wa kijamii wa facebook.

Aliyev aliandika '' Huseynov na timu ya soka ya Gabala wanapaswa kupigwa marufuku ya kushiriki mashindano yoyote barani Ulaya kwa kupeperusha bendera ya Uturuki

Tukio hilo lilitokea baada ya mechi baina ya ya mchujo ya ligi kuu ya Europa mnamo Agosti tarehe 6.

Kufuatia ripoti hiyo Aliyev alipokea vitisho kadha dhidi ya maisha yake. 

Aliyev alikutana na mtu aliyedai kuwa binamu ya mshambulizi huyo

Dadake aliwaambia waandishi wa habari kuwa mtu mmoja alimpigia simu na kutishia maisha yake.

Hatimaye alimpigia simu na kuomba wasameheane.
Inadaiwa kuwa Aliyev alikutana na mtu aliyedai kuwa binamu ya mshambulizi huyo akikusudia kuomba msamaha kwa maandishi yake.

Aliaga dunia jana alipokuwa akipokea matibabu katika wodi ya wagonjwa mahututi katika hospitali kuu ya Baku.

Yamkini mwandishi huyo alikuwa amekubali kukutana na mtu huyo kwa nia ya kwenda kunywa chai naye kama ishara ya mapatano na uwiano lakini alipofika sehemu waliokuwa wameahidi kukutana alivamiwa na kushambuliwa na takriban watu 6 waliokuwa wamemuwekea mtego.


Alipigwa vibaya na akakimbizwa hospitalini lakini aliaga dunia jana alipokuwa akipokea matibabu katika wodi ya wagonjwa mahututi katika hospitali kuu ya Baku. 

Rasim aliikashifu timu ya Gabala na mshambulizi wake Javid Huseynov
Hii si mara ya kwanza kwa Rasim kuingia matatizoni kutokana na uandishi wake.

Mwaka 2013,Rasim Aliyev alipigwa na maafisa wa polisi kutokana na ripoti yake.
Kichapo hicho kilinaswa kwa kamera na kuibua hisia kali miongoni mwa mashabiki wake nchini Azerbaijan

0 comments :

Top headlines

© 2011-2014 MICHEZONI. Designed by Alfred Meshack Bloggertheme9. Powered by Blogger.