Klabu ya Chelsea imetenga kitita cha pauni 15.5 milioni ili kuinasa saini ya Jose Callejon (pichani hapo juu) kutoka Napoli. Mchezaji huyo pia anawaniwa na klabu za Arsenal na Tottenham.
Mchezaji huyo amekuwa kwenye kiwango kizuri tangia ahamie klabuni hapo akitokea Klabu ya Real Madrid ambapo amefanikiwa kufunga mabao 28 katika mechi 32 alizocheza. Chanzo The Metro.
Klabu ya Bayer Leverkusen ya Ujerumani inawania huduma ya mchezaji Charles Aranguiz kutoka Sport Club Internacional ya Chile. Mchezaji huyo pia anawindwa na klabu ya Chelsea. The Telegraph.
Manchester United wako katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa winga Pedro kutoka Barcelona. Winga huyo amekuwa akihusishwa kuihama miamba hiyo ya Hispania baada ya kuona hali yake si nzuri klabuni hapo. Chanzo Mail Online
Bosi wa Real Sociedad, David Moyes anaimani kumpata kwa mkopo winga wa Manchester United, Adnan Januzaj mwenye umri wa miaka 19. Mchezaji huyo aling'ara sana wakati wa uatawala wa Moyes klabuni hapo. Chanzo The Express
Manchester United na Manchester City wako tayari kutoa pauni 20 milioni ili kumnasa kiungo wa Barcelona, Rakitic kutoka klabu ya FC Barcelona. Chanzo Daily Mirror.
0 comments :