Klabu ya Stand United ‘Wapiga debe’ wa Shinyanga imethibitisha kupitia mkurugenzi wake wa ufundi
kuwa klabu hiyo
ipo kwenye mazungumzo ya kumnasa kiungo wa Yanga ambaye kwa muda mrefu
amekosa nafasi ya kudumu ndani ya kikosi cha mabingwa hao wa msimu
uliopita.
Mkurugenzi
wa benhi la ufundi la Stand United Muhibu Kanu amesema, timu yao
imekaribia kumpata Hassan Dilunga kutoka Yanga ili ajiunge na Stand
United kwa ajili ya msimu ujao.
“Tulizungumza
tangu mwanzoni tulikuwa na mpango wa kumfuatilia mchezaji huyu, lakini
nafikiri tumeshakubaliana na kamati ya utendaji na mwenyekiti atakuja
kulizungumzia jambo hilo lakini ni kweli tunamazungumzo na Yanga kuhusu
kumsajili Dilunga”, Kanu amethibitisha.
“Mwenyekiti
wangu yupo hapo mjini (Dar es Salaam) yeye ndio analishughulikia jambo
hili na alipewa jukumu hilo na kamati ya utendaji kuhakikisha kwamba
analimaliza”, ameeleza.
“Sisi
kwa upande wetu kuna wachezaji ambao tulikuwa tumewapendekeza wanaotoka
kwenye timu nyingine lakini pia wengine wapo ambao wanatoka kwenye timu
yetu ya vijana ambao tutawapandisha kuja juu”, amesema.
“Kwahiyo
nafikiri mpaka tarehe ya mwisho ya usajili itakapotangazwa
tutawatangazia watanzania nani ambae ameingia na nani ambae ametoka na
ni wangapi ambao tumewapandisha kutoka kwenye kikosi cha vijana”,
ameongeza.
Lakini
katika hatua nyingine Kanu amekanusha taarifa zilizoanza kuzagaa kwamba
timu hiyo inampango wa kumsajili beki wa kulia wa Simba Nassoro Masoud
‘Cholo’ akisema uvumi huo hauna ukweli ndani yake na wala jina la Cholo
halipo kwenye mapendekezo ya wachezaji wanaotaka kuwasajili kwa ajili ya
msimu ujao huku akisisitiza kuwa, Cholo hana nafasi kwenye kikosi
hicho.
0 comments :